Font Size
Luka 11:34-36
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Luka 11:34-36
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
34 Namna unavyowatazama watu inaonesha kwa hakika jinsi ulivyo. Unapowatazama watu katika hali isiyo ya ubinafsi, inaonesha wazi kuwa umejaa nuru. Lakini unapowatazama watu katika namna ya uchoyo, ni wazi kuwa umejaa giza.[a] 35 Hivyo iweni waangalifu ili nuru iliyo ndani yenu usiwe giza! 36 Ikiwa umejaa nuru na hakuna sehemu yenye giza ndani yako, basi utang'aa, kama nuru ya kwenye taa.”
Read full chapterFootnotes
- 11:34 Kwa maana ya kawaida, “Taa ya mwili ni jicho lako. Unapowatazama watu bila kuwa na kinyongo, mwili wako wote unakuwa umejaa nuru. Lakini ikiwa jicho lako ni la uovu, mwili wako una giza.”
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International